Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, baadhi ya watu wanapofuatilia hali ya kusini mwa Lebanon katika mwaka huu hupata hitimisho lisilo sahihi na kutoa hoja potofu kwamba; ikiwa Lebanon iliushinda uvamizi wa Israel mwaka 2000, basi kwa nini eneo hilo hilo limekuwa tena uwanja wa moja kwa moja wa vita na kwa nini majeshi ya Israel yamevamia tena sehemu hiyo.
Hata hivyo, mtu anapoingia ndani zaidi katika kiini cha mzozo huu, huona kwamba ni muqawama na ustahimilivu huohuo wa watu wa Lebanon ambao unaendelea kuilinda nchi hii dhidi ya mashambulizi na dhidi ya kusambaratika kisiasa.
Utawala wa Kizayuni wenye mikono iliyolowa damu, tangu ulipoondoka katika sehemu kubwa ya ardhi ya Lebanon, umejaribu mara kwa mara—katika vita vya mwaka 2006 na katika matukio mengine kadhaa—kuvunja uwiano wa kuzuwia (deterrence) ambao Hizbullah imelazimishwa na utawala huo. Hata hivyo, majibu madhubuti ya Muqawama yameufanya kila mara urudi nyuma na kushindwa kufanikisha malengo yake.
Kwa upande mwingine, mabadiliko katika mfumo wa kijeshi wa “Israel” yamesababisha pia mabadiliko katika kanuni za mapambano zinazofuatwa na utawala huo wa bandia, kwa undani zaidi, adui wa Kizayuni hana tena wasiwasi mkubwa kuhusu makubaliano ya kubadilishana wafungwa au mikataba ya kusitisha vita, kwa sasa anaelekea zaidi katika kuanzisha vita vya wazi kwa lengo la kuangamiza vyanzo vyote ambavyo vinaweza kutishia asili na uwepo wa utawala huo wa kinyama, hata kabla havijajitokeza waziwazi.
Kwa kujibu hali hiyo, Muqawama wa Lebanon umeona kuwa ni muhimu kujibadilisha kulingana na mabadiliko ya utawala wa Kizayuni na kuweka kanuni mpya za mapambano, Kanuni hizo zimejengwa juu ya msingi wa kukubali changamoto ya vita vya wazi, kumzuia adui, na kuilinda nchi na uhuru wake.
Chanzo: Al-Manar Media Network.
Maoni yako